Sunday 2 August 2015

SERIKALI YASAINI MKATABA WA KUKUSANYA ZAIDI YA SH. MILIONI 12 KUPITIA MAPATO YA NDANI.

FE1
Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum (kushoto) akisaini Mkataba wa Makubaliano ya kukusanya Sh. milioni 12,362,969 za mapato ya ndani kwa mwaka wa fedha 2015/2016 hivi karibuni jijini Dar es salaam ambayo yanakusanywa kwa mara ya kwanza nchini. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bernard Mchomvu.

FE2
Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum (kushoto) akibadilisha hati ya mkataba wa makubaliano na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bernard Mchomvu ya kukusanya Sh. milioni 12,362,969 za mapato ya ndani kwa mwaka wa fedha 2015/2016 leo jijini Dar es salaam.
FE3
Baadhi ya viongozi na watendaji wa Wizara ya Fedha na TRA wakati wa hafla ya kusaini Mkataba wa Makubaliano ya kukusanya mapato ya ndani kwa mwaka wa fedha 2015/2016 ambayo yanakusanywa kwa mara ya kwanza nchini.

FE4

FE5

……………………………………………………………………………….
Na Eleuteri Mangi- MAELEZO
Serikaki imesainiana Mkataba wa Makubaliano ya kukusanya Sh. Milioni 12,362,969 za mapato ya ndani kwa mwaka wa fedha 2015/2016 ambayo yanakusanywa kwa mara ya kwanza nchini.
Mkataba huo wa makubaliano umesainiwa hivi karibuni jijini Dar es Salaam kati ya Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bernard Mchomvu kwenye hafla iliyohudhuriwa na baadhi ya viongozi na watendaji wa Wizara ya Fedha na TRA.
 “Hakikisheni mnakusanya mapato kama ilivyopangwa na kufikia malengo tuliyojiwekea katika kukusanya mapato ya ndani katika mwaka huu wa fedha” alisema Waziri wa Saada.
Waziri huyo aliwaasa watendaji wa TRA  kuwawekea wafanya kazi mazingira mazuri ya kutekeleza wajibu wao inavyopaswa na wanapokwenda kinyume na makubaliano ya kazi watawajibishwa kwa mujibu wa sheri, kanuni na taratibu za utumishi wa umma.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TRA Bernard Mchomvu alimhakikishia Waziri wa Fedha kuwa watafikia lengo walilokubaliana kukusanya na hata kuzidi kiwango hicho ambacho kimeainishwa katika bajeti ya Serikali.

No comments:

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!