Friday 29 May 2015

WANAOPATA AJALI ZA MABASI WALIPWE FIDIA

Waziri wa Sheria na Katiba, Asha- Rose Migiro
WAZIRI wa Sheria na Katiba, Asha- Rose Migiro amewataka Watanzania kutumia Sheria ya Madhara kudai haki zao baada ya kupata ajali ya basi.


Alisema Watanzania wanaweza kuanzisha shauri la madai katika kipindi cha miaka mitatu tangu wapate ajali hiyo iliyosababishwa na uzembe ili kulipwa fidia.
Sheria hiyo ya madhara ni zaidi ya Sheria ya Bima ambapo wananchi wanaopata ajali katika mabasi wanatakiwa kudai.
Migiro alikuwa anaongezea majibu ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Pereira Ame Silima kuhusu stahiki za aliyepata ajali katika basi lililoulizwa na Mbunge wa Kibaha Mjini Silvestry Koka (CCM) katika swali lake la nyongeza.
Naibu Waziri huyo alisema kwamba watu wanaopata ajali wanastahiki zao na ingawa hawafahamu ni lazima wadai fidia hizo kwani magari yanapokosa bima ni kosa la jinai.
Alisema serikali inataka watu wafahamu hivyo ingawa anajua watu wa bima hawaisemi wazi kwa kuhofia kupata hasara.
Akijibu swali la msingi la Mbunge huyo la taratibu zikoje katika ajali na muda unaotakiwa kupita kumaliza tatizo la ajali mahakamani, Naibu Waziri Silima alisema makosa ya Usalama Barabarani ni sawa na makosa mengine ya jinai na huendeshwa kwa mujibu wa Sheria ya Mwenendo wa Mashitaka na sheria inatoa mwongozo wa muda wa siku 60 kukamilisha upelelezi na uendeshaji wa kesi mahakamani.
Aidha alisema kwamba kunapotokea ajali dereva anatakiwa kusimama eneo la tukio na kutoa msaada kama maisha yake hayamo hatarini au kujisalimisha Polisi

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!