Friday 29 May 2015

ASILIMIA 42% YA WATOTO WAMEDUMAA TANZANIA

Asilimia 42 ya watoto wamedumaa nchini Tanzania hali inayosababishwa
na kukosekana kwa lishe bora yenye virutubisho hivyo hivyo kusababisha
udumavu na kuathiri afya ya akili.


Profesa Joyce Kinabo wa Chuo Kikuu cha Sokoine kilichopo mkoani
Morogoro amesema kuwa kukosekana kwa lishe bora kumekua kukiathiri
maendeleo ya taaluma kwa watoto na kuzorotesha maendeleo ya jamii kwa
ujumla.
Joyce akizungumza katika mkutano wa wa masuala ya Lishe uliondaliwa na
taasisi ya kimataifa ya chakula na lishe (FANUS), uliofanyika jijini
Arusha amesema kuwa kati ya watoto 100 watoto 42 wanakabiliwa na
tatizo la udumavu hivyo ameitaka jamii na serikali kutilia mkazo suala
la lishe bora na virutubisho ili kuondokana na tatizo hilo.
“Serikali na watunga sera wanapaswa kutambua uhusiano ulioko kati ya
lishe bora na maendeleo ya taifa,elimu ya lishe na virutubisho itolewe
kuanzia ngazi ya familia,jamii hadi kitaifa na pia mashuleni somo la
lishe lirudishwe ili kuchochea ustawi bora wa jamii na taifa” Alisema
Joyce
Amesema kuwa jamii ya wafugaji hususani wamasai wanakabiliwa na tatizo
la udumavu ,ukondefu na upungufu wa damu mwilini kwa kukosa kutumia
mboga mboga na matunda na vyakula vingine  kwani jamii hiyo hupendelea
maziwa na nyama.
“Asilimia 16% wana kimo kisicholingana na umri wao yote haya
yanasababishwa na lishe duni kwa baadhi ya watu” Alisema Profesa
Profesa Tola Atinmo wa chuo kikuu cha Ibadan nchini Nigeria kitengo
cha Virutubisho vya binadamu amesema kuwa haki ya kupata lishe na
virutubisho ni haki ya msingi ya kila binadamu kama ilivyoainishwa
kwenye mkataba wa haki za binadamu wa kimataifa wa mwaka 1948.
Ameishauri serikali kuhakikisha kuwa inaboresha masuala ya lishe,afya
na usalama wa chakula kwa raia wake .
Mkuu wa Mkoa wa Arusha ,Daudi Felix Ntibenda amesema kuwa mkutano huo
unatoa fursa kwa wataalamu wa masuala ya lishe nchini na viongozi
kujifunza masuala hayo muhimu katika maendeleo ya jamii.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!