A: Orodha ya Walimu na Mafundi Sanifu Maabara Ajira Mpya Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI inatangaza ajira ya wahitimu wa mafunzo ya
ualimu na mafundi sanifu maabara katika mamlaka ya Serikali za Mitaa kama ifuatavyo:-
i. walimu wa cheti (Daraja IIIA) kwa ajili ya shule za msingi 11,366;
ii. walimu wa stashahada 4,151 na shahada 12,490 kwa ajili ya shule za sekondari
iii. mafundi sanifu maabara 264 kwa ajili kusimamia maabara na kuandaa masomo
ya sayansi kwa vitendo katika shule za sekondari
B: Utaratibu Ajira Mpya kwa Walimu na Mafundi Sanifu Maabara
Kila mwajiriwa mpya anatakiwa kuzingatia yafuatayo:-
i. walimu wenye sifa waliohitimu mafunzo kwa mwaka wa masomo 2013/14
wamepangwa pamoja na walimu wa sekondari wa masomo ya sayansi na
hisabati waliohitimu miaka ya nyuma na wameomba kuajiriwa;
ii. kuripoti kuanzia tarehe 01 Mei hadi 09 Mei 2015 kwenye Ofisi za Wakurugenzi
wa Halmashauri kwa ajili ya kuajiriwa na kupangwa vituo vya kazi;
iii. kuwasilisha vyeti halisi vya taaluma ya kuhitimu mafunzo, elimu ya sekondari,
cheti cha kuzaliwa pamoja na nakala zake;
iv. hakutakuwa na mabadiliko ya vituo vya kazi; na
v. fedha za kujikimu kwa muda wa siku saba (7) na nauli ya usafiri wa magari
(ground travel) zitatolewa kwenye halmashauri husika baada ya kuripoti.
Imetolewa na
OFISI YA WAZIRI MKUU - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA
MITAA.
OFISI YA WAZIRI MKUU - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA
MITAA.
BONYEZA HAPA CHINI
1.KUSOMA ORODHA YA WALIMU WAPYA NGAZI YA CHETI KWA AJILI YA KUFUNDISHA SHULE ZA MSINGI2.ORODHA YA WALIMU WAPYA NGAZI YA SHAHADA NA STASHAHADA KWA AJILI YA KUFUNDISHA SHULE ZA SEKONDARI MASOMO YA SAYANSI NA HISABATI
3.ORODHA YA WALIMU WAPYA NGAZI YA SHAHADA NA STASHAHADA KWA AJILI YA KUFUNDISHA SHULE ZA SEKONDARI MASOMO YA SANAA NA BIASHARA
No comments:
Post a Comment