Sunday 1 February 2015

BILIONI 15 KUWALIPA WAFANYABIASHARA NA WAKULIMA WA MAHINDI



Serikali imetenga Sh. bilioni 15 na zimeanza kusambazwa kwa ajili ya kupunguza deni ambalo inadaiwa na wakulima na wafanyabiashara waliouza mahindi katika maghala ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya  Chakula.

Kauli hiyo ilitolewa na Naibu Waziri Kilimo, Chakula na Ushirika, Godfrey Zambi, wakati wa mkutano wa viongozi wa Vyama vya Ushirika mjini hapa.

Alisema Serikali inafanya kila liwezekanalo kuhakikisha wakulima na wafanyabiashara hao wanalipwa fedha hizo mapema ili ziwasaidie katika msimu huu wa kilimo.

“Hata katika kikao cha Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi kule Zanzibar, iliagiza kuwa lazima Serikali iwalipe madeni hayo haraka iwezekanavyo na ndiyo maana Hazina ikatenga kiasi cha Shilingi bilioni 15 kupunguza deni hilo, na tumeanza kuzisambaza,” alisema.

Hata hivyo, alisema bado wanaidai Serikali zaidi ya  Sh. bilioni  87 ambazo zitalipwa kwa awamu  ndani ya miezi minne. Aidha alisema  tatizo lililochelewesha malipo hayo kwa wakulima ni uhaba wa fedha Serikalini, ingawa alisema Serikali haina nia mbaya na wakulima na wafanyabiasha hao.

Kuhusu  pembejeo, alisema suala hilo  limewapa shida kutokana na baadhi ya kampuni yaliyopewa tenda na ushindwa kusambaza wakidai malipo   kwanza   kabla   ya   kusambaza.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!