Thursday 18 December 2014

POLISI WAWAZUIA WALIOPITIA JKT KUANDAMANA



Jeshi la Polisi  Kanda Maalumu jijini Dar es Salaam limezuia  maandamano ya vijana waliopitia mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na kuwataka Kuteua viongozi watano kwenda Ikulu kwa Rais Jakaya Kikwete kuwakilisha malalamiko yao.




Vijana haa ni waliopitia operesheni Mkapa, Utandawazi, Jiajili, Miaka 40, Kasi mpya, Maisha bora, Uadilifu pamoja na Kilimo kwanza toka mwaka 2000 hadi 2014.

Vijana hao  zaidi ya 300 walianza  maandamano hayo saa mbili asubuhi kutoka Jangwani  kuelekea Ikulu wakiwa wamebeba bendera zenye rangi nyekundu na vyeti walivyohitima mafunzo yao na walipofika eneo la Hospitali ya Ocean Road, polisi walizuia maandamano hayo na kuwataka kuchagua viongozi watakao wawakilisha.

 Askari hao  waliwataka wengine  kuondoka eneo hilo na kutafuta eneo lenye usalama kwenda kuwasubiri viongozi wao watakapotoka Ikulu na kuwaletea majibu.

Mmoja wa kiongozi wa mafunzo, Magesa Maijo, alisema lengo la maandamano yao ni kupeleka kilio  chao  kwa Rais  kutokana na kutopewa majibu sahihi kwa wizara husika.

CHANZO: NIPASHE

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!