Thursday 18 December 2014

MWANAUME MTANZANIA ALIYEUA WATOTO WAKE WAWILI NCHINI AUSTRALIA AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA



Charles Mihayo (36) mzaliwa wa Tanzania ambaye mwezi wa April 20 mwaka 2014 aliwaua watoto wake wawili wa kike huko nyumbani kwake Melbone Australia amehukumiwa kifungo cha maisha.



Taarifa zinadai kuwa baada ya Charles kuachwa na mke wake hasira zilimpanda bwana Mihayo na kuamua kufanya ukatili kwa watoto wake mwenyewe Savannah( 4)na  Indiana (3) alifanya hivyo kwa lengo la kumuumiza mke wake kwa lengo la kulipiza kisasi.

Inadaiwa kuwa aliwaua na kwa kuwakandamiza na mto baada ya kucheza nao.
Taarifa hizo zinaeleza pia kuwa siku ya mauaji hayo yalipofanyika, mama wa watoto hao aliwapeleka kwa baba yao bwana Mihayo, na baada ya kufika baba huyo aliwafanyia shopping ya nguo na viatu vipya kabla hajawaua.





Savannah,4, na Indianna, 3, enzi za uhai wao

Kabla ya kutenda ukatili huo kwa damu yake mwenyewe, bwana Mihayo aliwarekodi watoto wake kwenye video wakicheza muziki huku akicheza nao. Na katika video ambayo polisi waliiona ,alisikika akiwaambia binti zake wamuoneshe mama yao nguo alizowanunulia nao walifanya hivyo, na kisha bwana Mihayo akakaa mbele ya kamera na kusema "tutamuonyesha mama vitu vingine dakika dakika kumi zijazo" na kuendelea kucheza nao hadi alipowakandamiza na mto hadi kufa.

Baada ya kufanya mauaji hayo mihayo mwenyewe aliwapigia simu polisi na baada ya polisi kufika aliwaambia "tayari nimewaua"nimewaua watoto wangu inabidi mumuulize mama yao sababu .

Polisi waliwakuta watoto hao tayari wamefariki na huku wakiwa wamevalishwa nguo  na viatu vipya walivyonunuliwa na baba yao siku hiyo.

Licha ya kuhukumiwa kifungo cha maisha Charles Mihayo anatakiwa kutumikia kifungo cha miaka 31 kabla ya kupata haki ya kupewa msamaha.


1 comment:

Anonymous said...

Kukaa nje sana kunaharibu akili,huyo jamaa akapimwe akili zake tayari ni sita kasorobo,mgonjwa huyo.

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!