Thursday 18 December 2014

MAMA SALMA KIKWETE AZINDUA RASMI UMOJA WA VIKUNDI VYA WAMA KATIKA WILAYA YA KINONDONI‏



Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akipokewa na Mwenyekiti wa Umoja wa vikundi vinavyosimamiwa na WAMA katika wilaya ya Kinondoni (UWAMAKI), Ndugu Christina Emmanuel wakati alipowasili kwenye Chuo cha Usafirishaji kilichoko eneo la Ubungo kwa ajili ya ufunguzi wa umoja huo tarehe 18.12.2014.


Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akiangalia baadhi ya kazi zinazofanywa na wanavikundi wa UWAMAKI mara baada ya kuwasili kwenye sherehe ya uzinduzi wa vikundi hivyo tarehe 18.12.2014.




Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA, Mama Salma Kikwete akizindua rasmi umoja wa vikundi vya wama katika Wilaya ya Kinondoni katika sherehe ya kufana iliyofanyia kwenye Chuo cha Usafirishaji tarehe 18.12.2014.



Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akijumuika na wanavikundi vya UWAMAKI kusherehekea uzinduzi rasmi wa vikundi hivyo huko Chuo Cha Usafirishaji.

Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete akitoa hotuba yake mara baada ya kuzindua rasmi Umoja wa vikundi vya WAMA katika Wilaya ya Kinondoni katika sherehe zilizofanyika katika Chuo Cha Usafirishaji kilichoko eneo la Mabibo 

Baadhi ya wanachama wa umoja wa vikundi vya  WAMA katika wilaya ya Kinondoni wakisikiliza kwa makini hotuba ya mgeni rasmi Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati wa sherehe ya uzinduzi wa umoja wao 


Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipewa zawadi ya mkeka kutoka kwa wanachama wa vikundi vya WAMA katika wilaya ya Kinondoni, UWAMAKI, WAKATI WA SHEREHE ZA UZINDUZI WA Umoja wao 

PICHA NA JOHN  LUKUWI 

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!