Thursday 18 December 2014

ASILIMIA 97 WACHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2015

Jumla ya wanafunzi 438,960 kati ya wanafunzi 451,392 waliohiyimu elimu ya msingi mwaka huu wamechaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza mwakani.

Idadi hiyo ni sawa an asilimia 97 ya wanafunzi wote waliofanya mtihani huo.
Taarifa ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kwa waandishi wa habari leo imesema ufaulu huo umeongezeka kwa asilimia 1.08 ikilinganishwa na mwaka jana.
Hata hivyo, jumla ya wanafunzi 12, 432 waliofaulu, hawajapata nafasi ya kuchaguliwa kuendelea na masomo ay sekondari kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo uungufu wa majengi, hali inayowalazimisha kusubiri chaguo la pili litakalofanyika mapema mwakani.
Jumla ya wanafunzi 808,085 walisajiliwa kufanya mtihani wa taifa mwaka 2014 lakini ni wanafunzi 792,122 tu ndio waliofanya  mtihani, hiyo ikiwa ni asilimia 98.02% ya wanafunzi wote waliosajiliwa.
Taarifa ya Tamisemi inaongeza kuwa wavulana wanaongoza kwa kuchagaliwa zaidi ya wasichana ambapo jumla ya wavulana 219,964 wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza hiyo ikiwa ni sawa na asilimia 97.28 ya wanafunzi wote waliochaguliwa huku wasichana wakifikia 218,996 ambayo ni sawa asilimia 97.1 ya wanafunzi waliochaguliwa.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!