Saturday 22 November 2014

MENGI ZAIDI YA SAKATA LA VIDEO YA HOUSEGIRL ALIYEMTESA MTOTO WA MIAKA MIWILI KARIBU YA KUUA

Habari iliyotingisha na kuhuzunisha wengi jana ni ile video inaonesha  mtoto aliyekuwa  akiteswa karibu kufa na msichana wa kazi huko Uganda. 


Video hiyo iliyosambaa mitandaoni ikionyesha jinsi msichana huyo wa kazi alivyokuwa akimfanyia ukatili  wa kinyama mtoto wa miaka miwili, video hiyo ilionyesha mateso ya kipigo na pia jinsi alivyokuwa akimlazimisha mtoto kula chakula kwa namna ya kikatili.  Habari zinasema baba wa mtoto huyo aliamua kuweka kamera ya siri nyumbani hapo, baada ya kuona mtoto hakuwa na hali ya kawaida, na kwamba alikuwa anaonyesha dalili za unyonge na woga kwa msichana wa kazi. Habari zinasema mzazi huyo hakuamini alichokiona na ndipo alipoamua kurudi nyumbani na kumvamia msichana huyo na kumpa kipigo kitakatifu,mpaka majirani walipoingilia kati, na kumuokoa msichana huyo wa kazi


Inasemekana polisi walifika sehemu ya tukio na kumkamata mzazi huyo na kumtia nguvuni aliachiwa baada ya ushahidi wa video aliyowaonyesha, wakati huo msichana wa kazi akipelekwa Hospitali  mahututi kutokana na kipigo.

Akiongea kwa njia ya simu mama wa mtoto aliyejitambulisha kwa jina moja la Angela, amesema mtoto anaendelea vizuri baada ya kuruhusiwa toka hospitali alikopelekwa, na kwamba wanatarajia kurudi hospitalini wiki ijayo kwa ajili ya checkup ya mtoto huyo.

Angela ameongeza kuwa msichana huyo wa kazi aliyetambulika kwa jina la (Tumuhirwe) amekuwa mfanyakazi kwao kwa takriban siku 26 tu

Aliongeza kusema kuwa msichana huyo Tumuhirwe hali yake ni mbaya  kiasi cha kutoweza hata kula, anakula kwa kutumia mipira, na hana uwezo wa kutembea mwenyewe anatembea kwaWheelchair kutokana na kipigo toka kwa baba wa mtoto.

Tumuhirwe amefunguliwa kesi na atatumikia kifungo katika gereza la (Luzinda prison) na kesi yake inatarajiwa kusikilizwa tarehe decemba 8 2014.



USHAURI KWA WAZAZI WOTE

walezi wote kuwa makini katika kuwafahamu vizuri watu wanaowaachia watu wanaowaachia majukumu ya kuwalea watoto wao. Ni vyema kujipatia uhakika juu ya tabia za wasaidizi hawa wanaofanya kazi ya kushinda na kulea watoto wetu wakati wote ambao tunakuwa katika majukumu mengine ya kila ili kuweza kuendesha maisha yetu.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!