Wednesday 26 November 2014

MAANDAMANO YASAMBAA MJINI FERGUSON MAREKANI

Mamia ya waandamanaji waliandamana katika barabara za mji wa Ferguson na katika miji mingine 13

Idadi kubwa ya watu wamefanya maandamano mapya kuhusu uamuzi wa mahakama kutomfungulia mashitaka polisi mzungu aliyemuua kijana mwafrika mweusi katika mji wa Ferguson, Missouri.
Maandamano hayo yaliyofanyika kuanzia mjini New York hadi Seattle yalikuwa ya amani ingawa vurugu zilizuka mjini Oakland, California na katika miji mingine 13.
Kulikuwa na ghasia pia katika mji wa Ferguson huku polisi wakiwakamata watu 44 ingawa uharibifu mkubwa ulifanyika zaidi Jumatatu.
Darren Wilson, amesema haoni kama ana hatia yoyote kwa mauaji ya kijana Michael Brown
Afisa aliyemuua kijana Michael Brown anasema hakuwa na nia mbaya bali alikuwa anatekeleza majukumu yake kama mlinzi wa umma.
Afisaa huyo, Darren Wilson, aliyempiga risasi Michael aliyekuwa na umri wa miaka 18, aliambia, shirika la habari la ABC, kwamba wakati alipokuwa anapambana na kijana huyo kabla ya kumuua alihisi kama aliyekuwa anapimana nguvu na Hulk Hogan.
Afisa Darren aliambia mahakama kuwa anajua kuwa alifanya kazi yake vyema.
Polisi walilazimika kushika doria mjini Ferguson kutokana na vurugu zilizoanza tena Jumatano
Watu wengi katika mtaa wa Ferguson ambao wenyeji wake wengi ni waafrika weusi, walitaka afisa huyo ashitakiwe kwa kosa la mauaji lakini uamuzi wa mahakama ulifikia kuwa polisi huyo hatakabiliwa na kosa lolote kwa mauaji ya Michael.
Mawakili wa familia ya Brown waliuponda sana uamuzi wa mahakama wakisema haukubaliki kamwe na wala sio wa haki.
Magari ya polisi yalishambuliwa katika maandano yaliyozuka baadaye huku polisi wakilazimika kutumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji hao katika mji wa Ferguson wenye idadi ya watu 21,000 .

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!