Monday 20 October 2014

POLISI WAMUUA GAIDI WA MABOMU AKIWA MBIONI KUTOROKA

Tumekuwa tukipata taarifa zinazohusu matukio ya mauaji ambayo yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara nchini Tanzania, hali ambayo imeonekana kukithiri katika siku za usoni huku jeshi la polisi likitoa ahadi ya kufanya jitihada za kuhakikisha linawatia nguvuni wahusika wa matukio hayo.


Taarifa iliyonifikia hivi punde kupitia Radio One Breaking News inahusu kuuawa kwa mtuhumiwa namba moja wa kesi ya ulipuaji mabomu jijini Arusha, Yahaya Hassan Omar kwa kupigwa risasi na askari wa jeshi la polisi wakati alipojaribu kutoroka akiwa chini ya ulinzi.

Akitoa taarifa za kifo cha mtuhumiwa huyo kamanda wa polisi wa mkoa wa arusha Lebaratus Sabas amesema marehemu yahaya hassan omari hela maarufu kwa jina la (sensei) ambaye alikuwa anatafutwa kwa muda mrefu mtuhumiwa huyo alikamatwa wiki mbili zilizopita mkoani morogroro na kupelekwa arusha na bado alikuwa anaendelea kuhojiwa.

Kwa mujibu wa kamandaa sabas mtuhumiwa huyo ambaye kwa sasa marehemu yahaya, alikiri kuwa yeye ndiye alikuwa msimamizi mkuu wa matukio yote ya milipuko ya mabomu na ya kumwagia viongozi wa dini tindikali yaliyowahi kutokea mkoani arusha na maeneo mengine.


Aidha kamanda Sabas Amefaanua kuwa baada ya marehemu ambaye ni mtuhumiwa kukiri tuhuma hizo alikuwa bado anaendelea kutoa ushirikiano kwa kuanza kuonyesha vitendea kazi yakiwemo mabomu ambayo alidaiwa kuyaficha kondoa mkoani Dodoma.

Amesema wakati anasafirishwa walipofika eneo la kisongo katika barabara kuu inayoenda dodoma majira ya usiku alifanya jaribio la kutaka kutoroka na ndipo akapigwa risasi iliyomjeruhi mguu na kiuno na akafariki wakati anapelekwa hosipitali.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!