Tuesday 21 October 2014

MADEE NA WENZAKE KIZIMBANI LEO



MBUNGE wa Jimbo la Kawe (Chadema), Halima Mdee (35) na wenzake wanane wanaokabiliwa na mashitaka ya kutotii amri halali ya Jeshi la Polisi wanatarajia kusomewa maelezo ya awali leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.



Mdee, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha) pamoja na wanachama wenzake watasomewa maelezo hayo mbele ya Hakimu Mkazi Janeth Kaluyenda, kwa kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika.
Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Rose Moshi (45) mkazi wa Kinondoni B, Renina Peter maarufu kama Lufyagila mkazi wa Kinondoni Mkwajuni, Anna Linjewile (48) mkazi wa Mbezi Luis na Mwanne Kassim (32) mkazi wa Pugu Kajiungeni.
Wengine ni Sophia Fangel (28) mkazi Mbezi Beach, Edward Julius (25) mkazi wa Msasani, Martha Mtiko (27) mkazi wa Mikocheni A na Beatu Mmari (35) mkazi wa Kinondoni Mkwajuni.
Wanadaiwa kuwa Oktoba 4, mwaka huu, katika mtaa wa Ufipa, bila kuwa na uhalali walikiuka amri halali ya kutawanyika iliyotolewa na Mrakibu wa Polisi (SP) Emmanuel Tillf kwa niaba ya Jeshi la Polisi.
Katika mashitaka mengine inadaiwa siku hiyo katika eneo hilo, washitakiwa hao kwa pamoja, walifanya mkusanyiko usio halali kwa lengo la kutembea kwenda kwenye Ofisi ya Rais.
Washitakiwa walikana mashitaka na wapo nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti yaliyotolewa na Mahakama.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!