Thursday 30 October 2014

IDADI YA WALIOFARIKI KWA AJALI ARUSHA YAFIKIA 12.



Gari aina ya Toyota Hiace likiwa limeharibika vibaya baada ya ajali hiyo iliyotokea eneo la Makumira wilayani Arumeru jana.Wananchi wakishuhudia ajali hiyo.
Lori la mafuta lenye namba za usajili T582 ACR baada ya ajali hiyo.
WATU 12 wamefariki dunia katika ajali ya barabarani iliyotokea katika eneo la Makumira wilayani Arumeru baada ya basi dogo aina ya Hiace kugongana uso kwa uso na lori la mafuta.
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Arusha, Lebaratus Sabas amesema ajali hiyo ilitokea jana majira ya saa 10 jioni baada ya basi hilo dogo aina ya Toyota Hiace lenye namba za usajili T519 DBV lililokuwa likitokea jijini Arusha kwenda Usa River kuhama kwenye saiti yake na kukutana uso kwa uso na lori hilo la mafuta lenye namba za usajili T582 ACR lilikuwa linatoka Moshi kwenda Arusha.
Baadhi ya mashuhuda wa ajali hiyo wamesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa basi dogo na wameziomba mamlaka zinazohusika kuongeza adhabu kwa madereva wazembe.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!