Friday 24 October 2014

EBOLA YAGUNDULIKA NEW YORK

Daktari wa Marekani aliyekuwa akiwahudumia wagonjwa wa Ebola Nchini Guinea amepimwa na kukutwa na virusi vya ugonjwa huko katika hospitali ya ya mjini New York.

Dr Craig Spencer ambaye ni mmoja kati ya madaktari wasio na mipaka alianza kujisikia maumivu na homa siku chache tu baada ya kurejea Marekani akitokea Afrika Magharibi.
Siku ya Alhamisi wiki hii Craig alipelekwa hospitali kwaajili ya vipimo na kisha akatengwa kwa uchunguzi zaidi wa afya yake.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari Meya wa mji wa New York Bill de Blasio amesema watu hawapaswi kuwa na hofu kwani hatua zote mhimu zilifuatwa katika kumchunguza Dr.Craig na hadi alipobainika kuwa na maambukizi hayo.
Kubainika kuwa na virusi vya ugonjwa wa Ebola kwa Dr.Craig kunaongeza idadi ya waliobainika kuwa na ugonjwa huo nchini Marekani kutoka watatu na kufikia wagonjwa wanne.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!