Thursday 30 October 2014

BUNGE LA BUKINA FASO LACHOMWA MOTO

Waandamanaji wakilitazama bunge la Burkina Faso likiteketea kwa moto.


Waandamanaji hao wakishangilia baada ya kuchoma bunge.
Magari nayo yameteketezwa kwa moto.
WAANDAMANAJI nchini Burkina Faso leo wamechoma moto bunge la nchi hiyo kupinga kupitishwa kwa katiba itakayomruhusu rais wa nchi hiyo, Blaise Compaore kuongeza muda wa kukaa madarakani.
Rais Compaore anataka kuongeza muda zaidi katika utawala wake wa miaka 27 aliyotumia kuliongoza taifa hilo.
Taarifa kutoka Mji Kuu ya nchi hiyo, Ouagadougou, zinasema kuwa ukumbi wa chama tawala na makao makuu ya chama hicho cha Congress for Democracy and Progress yamechomwa moto pia.
Bunge hilo lilitaka kubadili katiba itakayomuwezesha Compaore, aliyeingia madarakani tangu mwaka 1987 ili aweze kuiongoza tena nchi hiyo mwakani.
Kumekuwepo kampeni za wapinzani wanaomtaka rais huyo kuachia ngazi na kutogombea katika uchaguzi wa mwaka ujao.
Kabla ya kuchomwa moto bunge hilo, polisi walilipua mabomu ya machozi kuwazuia waandamanaji waliokuwa wakielekea katika jengo la bunge hilo japo takribani watu 1,500 walifanikiwa kupenya na kulichoma bunge hilo.
Waandamanaji walionekana wakichoma nyaraka na kupora baadhi ya vifaa vya kompyuta huku magari yaliyokuwa nje ya jengo hilo nayo yakichomwa moto.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!