Tuesday 21 October 2014

ANGALIA KUKU WANAVYOONGEZEWA MADAWA HII HATARI SASA!

Hii tamaa ya wafanyabiashara, ambayo haijali hata afya na maisha ya wateja wao inasikitisha sana. Baadhi ya kampuni zinazouza kuku, kama hii iliyonaswa kwenye video, zimestukiwa kuwa zinawajaza kuku wembamba ili kuwanenepesha na kuwaongeza uzito kabla ya kuwauza, kwa kutumia kimojawapo au mchanganyiko wa yafuatayo:

  1. Maji ya chumvi
  2. Kemikali za kuongeza ladha, na za kulainisha.

  3.  Sababu kuku hao wamekuzwa haraka na kwa madawa, huwa hawana ladha ya asili
  4. Vimiminika/mabaki ya ng’ombe na nguruwe kutoka machinjoni
  5. Mwani au “seaweed” (mimea/magugu ya baharini)
    seaweed mwani Kuku wanavyoongezwa unene kichakachuaji ndani ya sekunde 10, kwa kutumia mabaki ya nguruwe na vingine [Video]
    Mwani (seaweed), mimea ya baharini ambayo ni mojawapo ya vinavyoongezwa katika uchakachuaji wa kuku

    Ukiachilia mbali utapeli kwa wateja, uchakachuaji huu pia unahatarisha afya zao, na kudhulumu haki zao za kidini, kama mamilioni ya Waislam, na Wayahudi nchini Uingereza wanaokula kuku bila kujua kuwa kuku hao wameshindiliwa mabaki ya nguruwe (soma: Chicken injected with beef and pork waste sold in UK.) katika mchakachuo huu unaoitwa “chiken plumping”(nenepesha kuku,) kuku hao huongezwa takriban asilimia 30 ya uzito wao wa awali; karibia theluthi nzima. Video chini inaonyesha mojawapo ya mbinu na kifaa vinavyotumika katika uchakachuaji huo





CRD: BLOG YA WANANCHI

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!