Wednesday 17 September 2014

UKATILI WA KIJINSIA WATISHIA MAISHA MKURANGA

VITENDO vya ukatili wa kijinsia kwa watoto na wanawake vimekithiri wilayani Mkuranga mkoani Pwani hatua inayopelekea asasi ya kiraia kutoa elimu ili kupunguza tatizo hilo.


Akizungumza na Tanzania Daima juzi mjini Kibaha, Mratibu wa Asasi isiyo ya kiserikali ya Kibaha Palarigo Centre (KPC) Mohamed Kiaratu alisema, matukio zaidiu ya kumi yametokea katika wilaya hiyo katika kipindi cha miezi tisa.
Alisema kuwa matukio hayo ni pamoja na ubakaji wa watoto, wanawake kuuawa kwa wivu wa mapenzi na uvamizi wa kituo cha polisi kulikosababisha kifo cha askari.
Kiaratu alisema, wanatafuta fedha ili kuweka kambi katika wilaya hiyo na kuweza kutoa elimu ili kutokomeza vitendo hivyo katika wilaya hiyo.
Alisema kuwa kwasasa asasi hiyo inaendesha mafunzo ya siku tatu ya kuelezea ukatili wa kijinsia, kwa washiriki 40 wanaotoka katika Halmashauri ya wilaya ya Kibaha mjini na Vijijini.
Alisema kuwa mafunzo hayo yanafanyika kwa ushirikiano wa KPC na Jumuiya ya kitengo cha jamii cha sheria kupinga unyanyasaji wa kijinsia kwa ufadhili wa fedha kutoka serikali kuu wizara ya katiba na sheria.
Alisema kuwa asasi hiyo ilianzishwa mwaka 1999 ikiwa na wanachama 24 ambapo kwa sasa ina wanachama 120, ikiwa na malengo ya kutoa elimu ya utetezi wa wanawake na watoto kwa haki za binadamu.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!