Wednesday 17 September 2014

NCHI ZA AFRIKA KUWA NA KIWANGO KIMOJA CHA BIDHAA


NCHI za Afrika zipo mbioni kuwa na kiwango kimoja cha bidhaa ambazo wataweza kuziuza katika nchi za Ulaya na Marekani.

Hayo yalibainika jana katika mkutano wa wataalam wa masuala ya viwango wa nchi zote za Afrika uliofanyika hoteli ya Legend Bahari Beach, jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Uledi Mussa, alisema hatua hiyo itakuwa ni fursa pekee kwa waafrika kutokana na ukweli kwamba kwa muda mrefu kumekuwepo vikwazo vya nchi hizo kufanya biashara katika masoko ya Ulaya.
Akitoa mfano, Uledi alisema utakuta bidhaa viwango vyote vya kimataifa imekidhi lakini inapoingia katika nchi ya Marekani inashindwa kuuzika kwenye maduka makubwa kutokana na viwango vyao walivyojiwekea.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Udhibiti wa Ubora kutoka Shirika la Viwango nchini (TBS), Tumaini Mtitu, alitaja mambo matatu ambayo yatajadiliwa kuwa ni uingizaji na usafirishaji bidhaa, vyakula kwa ajili ya mahitaji maalum na usalama wa chakula kwa ujumla.
Mtitu alisema pamoja na jitihada hizo, bado kuna changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwemo udogo wa maabara ya viwango ambapo kwa sasa wapo katika mchakato wa kuitanua.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!