Tuesday 30 September 2014

MAMA SALMA AWATAKA WAKE WA MARAIS NA VIONGOZI KUCHUKUA HATUA KUHAKIKISHA WATOTO, WASICHANA NA WANAWAKE WANAPATA ELIMU NA AFYA BORA.



Wake wa Marais pamoja na viongozi wametakiwa kuchukua hatua, kutumia sauti zao na nafasi yao ili kuhakikisha watoto, wasichana na wanawake wanapata elimu na afya bora na hivyo kujikwamua na hali ngumu ya maisha.

Mwito huo umetolewa jana na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati akiongea kwenye mkutano uliojadili jinsi gani Dunia ichukue hatua kwa ajili ya afya na uchumi wa wanawake na wasichana uliyofanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo Jengo la Umoja wa Mataifa (UN) mjini New York.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!