Friday 22 August 2014

WALIO OMBA MIKOPO HELSB KUJULIKANA

HESLB LOGO
BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu nchini (HELSB), imesema kuwa itatangaza rasmi majina ya wanafunzi waliokidhi vigezo vya kupata mkopo kwa mwaka wa masomo 2014/2015.

Hayo yamesemwa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Msaidizi wa Elimu na Mawasiliano, Cosmas Mwaisombwa, kwamba mchakato wa upokeaji maombi kupitia mtandao ulikamilika Julai 31.
“Tumepokea maombi 58,037 na mchakato wa uchambuzi na upangaji wa mikopo utakamilika baada ya majina ya wanafunzi waliodahiliwa na Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) yatakapowasilishwa rasmi kwenye bodi, kwani tunategemea taarifa muhimu kutoka kwenye tume hiyo ili kuepuka udanganyifu,’’alisema.
Mwaisombwa alisema kuwa pia serikali inatoa mikopo kwa wanafunzi wa nje waliopata udhamini wa kusoma nchi rafiki na Tanzania ili kuwawezesha kujikimu.
Aliongeza kuwa malipo ya mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi ambao hawajapata, yatakamilika kufikia wiki ijayo

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!