Friday 22 August 2014

AUAWA NA WANANCHI KWA TUHUMA ZA KUIBA PIKIPIKI KAHAMA




















 Baada ya kufikishwa hospital ya wilaya ya kahama kwa matibabu wasamaria wema wakimsaidia nesi kumpeleka kwa dakitari kwa huduma .
 
 
 
Kijana mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 30-32 ambaye hajafahamika majina wala makazi yake ameuawa kwa  kupigwa mawe, kisha kuchomwa moto na wananchi wanaodaiwa kuwa na hasira, baada ya kumtuhumu kutapeli pikipiki.

Tukio hilo limetokea jana  majira ya saa tano asubuhi katika mtaa wa Nyihogo, eneo la Mnazi Mmoja, Barabara ya Tabora Karibu na Ofisi za halmashauri ya Mji wa Kahama Mkoani Shinyanga.

 Mtuhumiwa huyo ambaye kwa sasa ni marehemu inadaiwa alikodisha Pikipiki hiyo  zaidi ya Miezi mitatu iliyopita katika eneo la Maegesho ya Daladala za Pikipiki katika Lango kuu la hospital ya Wilaya hiyo.

Aidha Mmiliki wa Pikipiki hiyo ambaye hajafahamika mara moja wala namba ya  pikipiki, inadaiwa alimkamata  maeneo ya mtaa wa Shunu Kata ya Nyahanga ambapo aliamua kumpeleka katika kituo cha polisi  akiwa amemfunga kamba.

 Baada ya wananchi kuona mtuhumiwa amefungwa kamba ndipo wakamuuliza mmiliki huyo ambaye aliwaeleza, na ghafla wananchi wakaanza kumshambulia kwa mawe na kisha kumchoma Moto.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa shinyanga Justus kamugisha Amedhibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa ni kweli tukio hilo limetoka jana majira ya asubuhi saa 5 kijana moja ambaye jina lake alikuweza kufahamika mara moja alikuwa amekamatwa na mwanachi moja ambapo alikuwa ametoroka na pikipiki yake maeneo ya nyahanga wilayani kahama .

Aidha kamanda kamugisha alizidi kuelezea kuwa pamoja na tukio hilo kutokea kwa kijana huyo  jeshi la polisi linawatafuta watu wote walifanya mauji hayo

MATUKIO KATIKA PICHA:


 Hapa ni baadhi ya mwananchi wakijalibu kumtambua kijana huyo.
 Twendeni sasa
 Jamaani nakufa hayo ni maneno ya huyo kijana hakisema kwa tabu sana

 Haya kaa vizuri kaka umekwisha fika hapa hospitali
 
CHANZO KIJUKUU BLOG

1 comment:

Anonymous said...

aziz bilalIgår 16:50


1


Yale yale tena ya watu kujichukulia sheria mikononi mwao,siju lini hii mob justice itakwisha Tanzania.

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!