Wednesday 28 May 2014

RAIS KIKWETE AIPONGEZA TIMU YA WATOTO KWA KUNYAKUWA KOMBE LA DUNIA


Rais Kikwete afurahishwa jinsi watoto hao walivyonyakua kombe hilo la dunia.


"Mmetuwakilisha vyema, ninawapongeza sana, pia mmewapa moyo watoto wengine wote wenye vipaji maalum lakini hawakubahatika kuwa na makazi rasmi, hongereni sana" Rais amesema.


Timu hiyo ya watoto wenye umri chini ya miaka 16 ilipangwa kundi la 2 ambapo pia zilikuwapo timu kutoka Nchi za Argentina, Nicaragua,Philippines na Burundi.

Makundi yaliyopangwa yalikuwa matatu.
Tanzania iliingia nusu fainali kwa kuwa mshindi wa pili na pia kumenyana na Marekani na kuichapa mabao 6-1 na baadae kuitoa Burundi kwenye fainali kwa mabao 3-1.

"Hongereni kwa kujituma na kucheza kwa ustadi". Rais amesema na kuwaasa watoto "ongezeni bidii, nidhamu na mazoezi ya kutosha na hakika mtafanikiwa zaidi na kulibeba jina la Tanzania mbali zaidi ya hapa katika ulimwengu wa soka duniani, kwani hakuna kisichowezekana kama mtazingatia maelekezo, mafunzo, bidii na nidhamu ya yote mnayofanya" Ameongeza Rais Kikwete.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!