Tuesday 23 July 2013

HATIMAYE MTOTO WA KIFALME AZALIWA



Subira yavuta kheri na kheri imevutika nchini Uingereza.
Mkewe Prince William, Kate Middleton hatimaye kajifungua mwanawe wa kwanza wa kiume ambaye pia atakuwa mtoto wao wa kwanza . Kate alikimbizwa hospitali mjini London kwa gari akiwa ameambatana na mumewe.
Shangwe vifijo na hoi hoi zimetanda katika jiji la Uingereza na vitongoji vyake baada ya mke wa mwana mfalme Kate kujifungua mtoto wa kiume leo Jumatatu 22-07-2013 saa 10.24 jioni .Mtoto wa kifalme huyo anaingia katika kizazi cha nne cha kifalme.
Kate, aliyejulikana awali kama Catherine Duchess wa Cambridge, amejifungua mtoto huyo wa kiume katika hospitali ya St.Mary huko jijini London. Mtoto huyo atakuwa wa tatu katika mstari wa kupata ufalme kutoka kwa babu yake, mwana mfalme Charles, na Baba yake William.
“Mimi na mke wangu tunafuraha kubwa sana kwa ujio wa kuzaliwa mjukuu wetu wa kwanza” alisema Charles kwenye tamko lilotolewa na msemaji wa familia ya kifalme.
“ Maisha ya kuwa babu na bibi wa mjukuu ni ya kipekee sana katika maisha ya mtu. Na leo nina furaha sana kuwa babu kwa mara ya kwanza na tunasubiria kwa hamu kubwa sana kumwona mtoto aliyezaliwa” Alisistiza Charles kwenye tamko hilo.
Shangwe na hoi hoi zimesikika nje ya eneo la Lindo Wing ambapo ipo hospitali ya St. Mary baada ya tamko hilo kutolewa. Watu wazidi kumiminika kuelekea katika kasri ya kifalme kupate habari zaidi juu ya ujio wa mtoto wa kiume aliyezaliwa.
CHANZO:www.dailymail.com

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!